Basi bwana miaka miwili iliyopita  nilipata nafasi ya kwenda Mwanza kwa mara ya kwanza! Ilikuwa ni kama ‘dream come true’ hivi kwasababu ni moja ya sehemu ambazo nilikuwa nataka sana kuzitembelea.

Toka mwaka huo nimeenda Rock City mara nyingi sana na hakuna sehemu napenda kutembelea kama Kisiwa cha Saanane! Mandhari ya Kisiwa hiki hayaelezeki. Ni dunia ambayo wanyama, binadamu na mimea wanaishi kwa pamoja!

Kisiwa hiki cha kipekee cha Saanane kilikuwa kikimilikiwa na mzee Saanane ambaye alikuwa mfugaji na baadae alimua kuwa mkulima. Mzee Saanane alihamishwa na serikali na kwenda kisiwa kingine cha jirani na Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ikaanzishwa. Hifadhi hii ilianzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama mnamo mwaka 1964 na lengo la kuanzishwa kwake lilikuwa ni kuhamasisha uhifadhi na kuelimisha jamii juu ya uhifadhi.

Mwaka 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki. Wanyama wanaopatikana katika Hifadhi hii ni pamoja na Mbogo, Digidigi, Pongo, Swala, Ngiri, Pundamilia, Nyoka, Mamba na aina mbalimbali za ndege. Pia kuna Simba wawili jike na dume ambao wamefungiwa sehemu maalumu ili kuifanya Hifadhi hii kuwa sehemu salama.

Bustani hii iligeuzwa kuwa Game Reserve yaani pori la akiba mwaka 1991 na kupitishwa rasmi kuwa Hifadhi ilipofika mwaka 2013 na kuifanya hifadhi ya taifa ya Kisiwa cha Saanane kuwa hifadhi ndogo zaidi nchini Tanzania.

Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane inafikika kwa urahisi sana kutokea Mwanza mjini kwa boti ambayo inatumia dakika 5 tu kukatiza katikati ya Ziwa Victoria na kuifanya safari ya kuifikia hifadhi hii kuwa ya kipekee Zaidi.

Kuna shughuli nyingi za kitalii unaweza kuzifanya unapokuwa katika hifadhi hii Kisiwa Cha Saanane ikiwa ni pamoja na kuangalia wanyama, kukwea miamba, kutizama ndege, kupiga makasia na kutazama machweo ya jua.

Obviously hii picha ni zamani… nimekula zangu pozi Kisiwani 🙂

Hifadhi hii inakupa nafasi ya kujifunza jinsi binadamu na wanyama wanavyoweza kuishi kwa pamoja kwa kuheshimu mipaka na taratibu zilizowekwa kama kutowakurofisha au kuwalisha chakula. Kwa mara ya kwanza niliweza kukaa kusimama karibu na wanyama bila kuogopa nah ii ilinipa nafasi ya kuona umuhimu uliopo wa jamii kujifunza juu ya uhifadhi na kujali maisha ya wanyama na jinsi shughuli mbalimbali za kibindamu zinaweza kuathiri maisha yao.

Gharama za kungia katika hifadhi hii ni ndogo sana kwa watanzania nah ii inatoa nafasi kwetu wazawa kutembelea hifadhi za taifa na kuwa sehemu ya kutangaza vivutio vilivyopo nchini kwetu lakini pia kujifunza.

Until next time,

Jane 🙂

2 thoughts on “Hifadhi ya Kisiwa cha SaaNane, Mwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *